NEW
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara, Yusuph Manji na wenzake watatu imeahirishwa hadi Agosti 9 mwaka huu itakaposomwa tena.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Huruma Shaidi ameahirisha kesi hiyo mara baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kueleza kuwa mshtakiwa wa kwanza, Yusuph Manji alikuwa Mahakama Kuu.
Wakili Kishenyi ameiomba mahakama hiyo kusoma tena kesi hiyo Jumatano Agosti 9 mwaka huu, pia upande wa utetezi ukiunga mkono ombi hilo huku upelezi wa kesi hiyo ukiwa haujakamilika.
Aidha, katika kesi hiyo, Manji na wenzake wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya sheria ya uhujumu uchumi na usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya shilingi milioni 200 na mihuri.
Hata hivyo, mbali na Manji washtakiwa wengine walikuwepo mahakamani hapo ni Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere ambao kwa pamoja wamerudishwa rumande.
0 Comments