Breaking News:

Top Ad

//

Chelsea yashindwa kutamba mbele ya Inter Milan


SPORTS

Chelsea wamemaliza ziara yao ya kujiandaa na msimu ujao kwa kuambulia kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Inter Milan katika mchezo uliopigwa leo hii nchini Singapore.
Stevan Jovetic alitangulia kuipatia Inter Milan katika dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati baada ya Cesar Azpilicueta kumuangusha Jovetic katika eneo  la hatari.
Mchezaji anayewindwa kwa karibu na klabu ya Manchester United Ivan Perisic aliifungia bao la pili Inter Milan katika dakika ya 53 kabla ya Geoffrey Kondogbia wa Inter Milan kujifunga dakika ya 74.
Bao alilojifunga Geoffrey Kondogba ni moja kati tukio la kushangaza kutokana na mchezaji huyo kupiga mpira kutoka umbali wa mita 45 ulioelekea langoni mwake na kutinga wavuni.
Katika mchezo huo kocha Antonio Conte alipanga kikosi cha nguvu huku katika safu ya ushambuliaji akimuanzisha mshambuliaji wake mpya Alvaro Morata aliyecheza na mbeligiji Michy Batshuayi pamoja na mbrazili Willian.

Post a Comment

0 Comments