Breaking News:

Top Ad

//

conte kaiponda kikosi cha Tottenham Hotspurs






 Katika  kile kinachoonekana kama kukidharau kikosi cha Maurico Pochettino kocha wa klabu ya Chelsea Antonio Conte amehoji matarajio ya klabu ya soka ya Tottenham akisema kuwa klabu hiyo ina malengo na matarajio kwa kiasi kidogo ukilinganisha na wapinzani wake katika Ligi kuu.
Conte amesema Tottenham isiposhinda ubigwa au isiposhiriki kwenye  ligi ya mabigwa Ulaya UEFA sio jambo la kushangaza kwa vilabu kama Chelsea, Manchester City, Manchester United na Arsenal
Kama lengo lako ni kushinda kombe na kufanya vizuri kwenye mashindano ya UEFA inabidi ununue wachezaji wazuri kwa bei kubwa la sivyo utaendelea kuwa kweye ngazi ya chini kila siku”Alisema Conte.
Mpaka sasa Klabu ya Tottenham Hotspurs haijafanya usajili licha ya kumuuza beki wake Kyle Walker kwa paundi milioni 50 katika klabu ya Manchester City.
Tottenham ilimaliza nafasi ya Pili Msimu uliopota nyuma ya Klabu ya Chelsea ambao walishinda ubingwa na kuifanya timu hiyo kukata tiketi ya kushiriki michuano ya UEFA msimu huu ambayo ufunguzi wake ni Agosti 8 mwaka huu 2017.

Post a Comment

0 Comments