Breaking News:

Top Ad

//

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 27.07.2017


Paris Saint_Germain wana uhakika wa kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 198 wa Neymar, 25, kutoka Barcelona katika siku 15 zijazo. (L’Equipe)
Barcelona watajaribu kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, iwapo watampoteza Neymar anayedhaniwa kuelekea PSG. (TalkSport)
Philippe Coutinho ameiomba Liverpool ruhusa ya kuondoka, na tayari amefikia makubaliano ya maslahi binafsi na Barca. (RAC1)
Barcelona watawapa Liverpool kiungo Ivan Rakitic kama sehemu ya mkataba wa kumchukua Philippe Coutinho. (Don Balon)
Hatua ya Real Madrid kutaka kumsajili mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe, 18, huenda ikasababisha winga Gareth Bale, 28, kwenda Old Trafford. (Indepenent)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema klabu yake ina fedha za kutosha za kupambana na Real Madrid katika kumsajili Kylian Mbappe. (Mail)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameonesha dalili kubwa kuwa Zlatan Ibrahimovic, 35, atasaini mkataba kubakia Old Trafford. (Times)
Manchester United wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 44.6 kumtaka mchezaji wa RB Leipzig Emil Forsberg. (Daily Star)
Iwapo Kylian Mbappe atasaini kwenda Real Madrid, Manchester United watataka kumsajili Gareth Bale, huku taarifa kutoka Old Trafford zikisema kuna ‘nafasi kubwa’ ya Bale kwenda Old Trafford. (The Independent)
Manchester United bado wanataka kumsajili kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic, 28, na wanaamini wataweza kuwashawishi Chelsea kuwauzia kwa zaidi ya pauni milioni 40. (Independent)
Licha ya kuhusishwa na kuhamia Manchester United, Ivan Perisic atapewa mkataba mpya kubakia Inter Milan, ambao hawaamini Man Utd watakubali kutoa fedha zaidi na kukubali mkataba ambao utamhusisha Anthony Martial kwenda Inter. (Football Italia)
Manchester United watamgeukia Emil Forsberg wa RB Leipzig iwapo watamkosa Ivan Perisic. (Calciomercato)
Gareth Bale amekataa nafasi ya kuhamia Arsenal, ambao wanamtaka ili kuziba nafasi ya Alexis Sanchez. (Don Balon)
Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 25, anataka kubakia England iwapo ataondoka Emirates. (ESPN)
Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 45 wa kiungo wa Monaco Thomas Lemar. (Sun)
Thomas Lemar huenda akabakia Monaco, baada ya makamu wa rais wa klabu hiyo Vadim Vasilyev kusema kiungo huyo hauzwi. (Metro)
Arsenal watamkosa kiungo wa Barcelona Arda Turan, huku Galatasaray ya Uturuki ikikaribia kukamilisha usajili wake. (Mirror)
Kiungo wa Borussia Dortmund Mikel Merino, 21, anakaribia kujiunga na Newcastle. (Evening Chronicle)
Beki wa kati Mamadou Sakho, 27, hajajumuishwa kwenye kikosi cha Liverpool cha wachezaji 30 watakaocheza mechi tatu za kirafiki nchini Ujerumani. (Liverpool Echo)
Chelsea wanataka kukopa pauni milioni 500 ili kujenga uwanja wao mpya, badala ya kutegemea fedha za Roman Abramovic. (Times)
Chelsea wanazungumza na wadau mbalimbali kuhusu uuzaji wa haki za jina la uwanja mpya, ingawa klabu hiyo inasisitiza kuwa jina la Stamford Bridge litapewa heshima yake kwa njia moja ama nyingine. (Evening Standard)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema angepewa nafasi ya kununua mshambuliaji yoyote yule duniani angemnunua Harry Kane, 23, wa Tottenham. (Daily Mail)
AC Milan wamekuwa na mawasiliano na wakala wa Diego Costa kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Chelsea. (Daily Express)
Wakurugenzi wakuu wa AC Milan Marco Fassone na Massimo Mirabelli wamekutana na wakala Jorge Mendes kumzungumzia Cristiano Ronaldo. Vigogo hao wa Milan wanataka wajulishwe mara tu Ronaldo atakapoweza kupatikana ingawa hakuna majadiliano yoyote kwa sasa. (Sky Sports)
Tottenham wanamnyatia kiungo wa Benfica Ljubomir Fejsa, 28. (Sun)
Meneja wa Everton Ronald Koeman anataka kusajili wachezaji wengine watatu- beki wa kati, mshambuliaji na kiungo mshambuliaji wa Swansea Gylfi Sigurdsson. (Mirror)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili 
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki njema.
Young Ndava

Post a Comment

0 Comments