Breaking News:

Top Ad

//

MAN UNITED YA AMBULIA KIPIGO MBELE YA WABABE WA SPAIN




SPORTS
MAN UNITED YA AMBULIA KIPIGO MBELE YA WABABE WA SPAIN
Baada ya Manchester United kushinda michezo yao yote ya kujiandaa na msimu wa ligi hatimaye usiku wa kuamkia leo wamekutana na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wababe wa Hispania timu ya Barcelona.
United ambao wako kwenye kiwango kizuri kwa sasa walikuwa uwanjani kupambana na Barcelona katika mchezo wao wa mwisho barani America.
Katika ya dakika ya 31 mchezaji anayezungumzwa sana katika yombo vya habari kwa sasa Neymar Dos Santos aliipatia Barcelona bao pekee baada ya kupokea pasi nzurikutoka kwa Lionel Messi.
Manchester United kupitia kwa Lukaku na Rashford walijitahidi sana kulishambulia sana lango la Barcelona lakini umahiri wa golikipa Jasper Cillessen ulizizima jitihada za United.
Baada ya kumaliza ziara ya Marekani Man United sasa wanarudi barani Ulaya kwa michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Vilarenga nchini Norway na mchezo dhidi ya Sampdoria kabla ya kukutana na Real Madrid katika fainali ya Super Cup.




Post a Comment

2 Comments