TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 31.07.2017
Jose Mourinho amesema Nemanja Matic, 28, “anataka sana” kuondoka Chelsea na kujiunga na Manchester United. Tayari United wamekubali kutoa pauni milioni 40 na wanatarajia kukamilisha usajili huo siku chache zijazo. (Sky)
Jose Mourinho amesema Nemanja Matic, 28, “anataka sana” kuondoka Chelsea na kujiunga na Manchester United. Tayari United wamekubali kutoa pauni milioni 40 na wanatarajia kukamilisha usajili huo siku chache zijazo. (Sky)
Beki wa kulia wa Paris Saint-Germain Serge Aurier amekubali kujiunga na Manchester United, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ufaransa. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ameruhusiwa kuondoka na meneja Unai Emery. (Sky Sports)
Alexis Sanchez anafikiria kuwasilisha ombi la kuondoka Emirates ili kulazimisha uhamisho wake kwenda Manchester City. Sanchez anataka sana kuondoka, na Pep Guardiola yuko tayari kufanikisha usajili wake. Sanchez anataka mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki, na Arsenal wako tayari kutoa 300,000. (Daily Mirror)
Southampton wana matumaini kuwa Virgil van Dijk atabadili mawazo na kurejea mazoezini na kikosi cha kwanza wiki hii. Southampton hawataki kumuuza beki huyo anayenyatiwa na Liverpool. (Daily Echo)
Barcelona huenda wakaamua kumgeukia Mesut Ozil, 28, iwapo watashindwa kumpata kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho. Huku hatma ya Neymar kwenda PSG ikiwa inazungumzwa, Barca wanatafuta mchezaji wa kuziba pengo lake. (Don Balon)
Cristiano Ronaldo hataki Real Madrid imnunue Kylian Mbappe kwa sababu huenda kinda huyo ‘akamfunika’ na kuathiri nafasi ya kushinda Ballon d’Or. (Diario Gol)
Matumaini ya Liverpool kumsajili Naby Keita yanazidi kupata wakati mgumu baada ya Inter Milan nayo kuingia katika harakati za kumtaka kiungo huyo. (CalcioMercato)
Arsenal na Tottenham wamepeleka maskauti wao kumtazama mshambuliaji kinda wa Caen, Yann Karamoh, ambaye ametajwa kuwa kama “Kylian Mbappe mwingine”. Chipukizi huyo anafuatiliwa pia na Forentina na AC Milan na Inter Milan. (Sunday Mirror)
Chelsea wanapanga kutaka kumchukua kinda wa Celtic, Karamoko Dembele, 14. (The Sun)
Kiungo wa Everton Ross Barkley atalazimika kupunguza mshahara anaotaka iwapo anataka kujiunga na Tottenham ambao wapo tayari kumlipa pauni 120,000 kwa wiki, sawa na ambazo amezikataa Everton. (Mirror)
Everton watashikilia bei ya pauni milioni 35 kumuuza Ross Barkley licha ya kuwa mkataba wake utamalizika baada ya mwaka mmoja. (Mail)
Barcelona watawashitaki PSG kwa UEFA kwa kukiuka kifungu cha fedha hata kama hawatolipa pauni milioni 197 za kutengua kifungu cha uhamisho cha Neymar. (El Larguero)
PSG wana uhakika wa kumsajili Neymar, na tayari wanapanga jinsi ya kumtambulisha mchezaji huyo kwa mashabiki. (ESPN)
West Brom wanamtaka beki wa zamani wa Arsenal, Thomas Vermaelen, 31, ambaye alihamia Barcelona miaka mitatu iliyopita. (Sky Sports)
Meneja wa Bacelona Ernesto Valverde anataka kumpa namba Thomas Vermaelen msimu huu baada ya kufurahishwa na kiwango alichoonesha kwenye mechi za kujipima nguvu. (AS)
Wachezaji wa Manchester City wanazungumzia waziwazi kuwasili kwa Alexis Sanchez kutoka Arsenal kwa mkataba wa pauni milioni 50. (Manchester Evening News)
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema wachezaji kama Alexis Sanchez na Mesut Ozil ambao wanaingia katika mwaka wa mwisho wa mikataba yao ndio “wazuri zaidi” kwa sababu watataka kuonesha kiwango cha juu. (Sun)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho hana mpango wa kumtoa kwa mkopo kiungo Andreas Pereira, 21, baada ya mchezaji huyo kuonesha kiwango katika mechi za kujipima nguvu. (Sun)
*Picha ya Nemanja Matic akiwa amevaa jezi ya Man Utd ambayo imezagaa mitandaoni na kutumika hata na gazeti la Star Sport haijathibitishwa bado kama ni rasmi la halisi.
*Sun Sport ukurasa wa michezo inasema Arsene Wenger huenda akapoteza wachezaji wenye thamani ya pauni milioni 125 bila kupata hata senti kwa kuwa watatu hao mikataba yao inaisha mwakani na wataondoka bure iwapo hawatauzwa msimu huu na ikiwa hawatasaini mikataba mipya.
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki njema.
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki njema.
0 Comments