KLABU ya Juventus imekubali kulipa dau la paundi milioni 63 kumnunua beki wa Ajax, Mholanzi Matthijs de Ligt mwenye umri wa miaka 19. (De Telegraaf - in Dutch)
West Ham wanataka kulipa kitita cha paundi milioni 10 ili kumsajili kiungo wa kati wa Equatorial Guinea Pedro Obiang, 27, licha ya klabu za Itali kama vile Bologna na Sassuolo kuonyesha hamu ya kumnunua mchezaji huyo. (Sun)
West Ham ipo katika mazungumzo na klabu ya Eintracht Frankfurt ili kumsani mshambuliaji wa timu hiyo, Mfaransa Sebastian Haller(25) kwa ada ya paundi milioni 40. (Sky Sports)
Tottenham inatarajia kuwasilisha ombi la kumsajili kiungo wa kati wa Leeds, Muingereza Kalvin Phillips, ambaye klabu hiyo ya York Shire inasema ana thamani ya paundi milioni 30. (Mirror)
Manchester United bado ipo katika mpambano wa kuwania saini ya kiungo wa kati wa Newcastle, Muingreza Sean Longstaff kutoka Newcastle licha ya klabu hiyo kutokubaliana juu thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Sky Sports)
Lakini bei ya Newcastle ya paundi milioni 50 inaweza kuifanya United kujitoa katika mpambano huo (ESPN)
Manchester United wameongeza dau la paundi milioni 30 ya thamani ya kiungo wake, Mfaransa Paul Pogba, 26, na sasa wanataka dau la paundi milioni 180 kumuuza mchezaji huyo waliyemnunua kwa dau la paundi milioni 89 mwaka 2016 kutoka Juventus.(Star)
Juventus wamesitisha hamu yao ya kutaka kumsajili Pogba, wakitoa fursa kwa Real Madrid kumsaini mchezaji huyo wa Ufaransa. (Mail)
Manchester United huenda ikamsajili beki wa Monaco na Ufaransa 19 Benoit Badiashile,ambaye pia anawaniwa na Wolves - iwapo watamkosa beki wa Leicester City, Muingereza Harry Maguire, 26. (L'Equipe, via Express)
Inter Milan huenda wakalazimika kulipa takriban paundi milioni 90 ili kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji na Man United Romelu Lukaku, 26, msimu huu (Telegraph)
Arsenal inataka kulipwa dau la paundi milioni 8.8 ili kumuuza nahodha wake, beki Mfaransa Laurent Koscielny, 33 ambaye anataka kuondoka katika klabu hiyo na ambaye alikataa kuungana na wenzake kuelekea Marekani kwa mechi za maandilizi ya msimu ujao. (London Evening Standard)
Arsenal imeongeza nguvu ya kupata saini ya beki wa Benfica, Mreno Ruben Dias, 22, hiyo ni kutokana na maamuzi ya hivi karibuni ya Koscielny (Mail)
0 Comments