Breaking News:

Top Ad

//

GARI;linalo tumia solar la gunduliwa


Mwanafunzi mmoja nchini Kenya ameunda gari linalotumia kawi ya jua, gari ambalo limekuwa likiwavutia watu sana mtaani kwake, na mtandaoni.

Samuel Karumbo, 30, ni mwanafunzi katika chuo cha mafunzo anuwai cha serikali mjini Kitale, Magharibi mwa Kenya lakini ameliunda gari lake katika eneo la Langas, Eldoret si mbali sana na mji wa Kitale.

Anasema gari lake, ambalo lina mitambo mitatu ya sola iliyobandikwa, linaweza kusafiri umbali wa kilomita 50 kwa siku.

Mitambo hiyo inaweza kuzalisha kawi ya jumla ya wati 260.

Karumbo anasema mchana, sola huchukua nishati ya jua na kuibadilisha kuwa umeme ambao unahifadhiwa kwenye betri ambazo ndizo zinazotumiwa moja kwa moja kuliendesha gari hilo na pia wakati jua halijawaka sana.

Gari hilo lina uzani wa kilo 120 na kwenye mteremko hutumia mvuto wa nguvu za ardhi badala ya umeme. Nguvu hutumia tu kwenye kupanda milima au maeneo yenye miinuko.
Bw Karumbo, ambaye jina lake la utani ni Gadget Man, anasema analenga kuwahamasisha watu kutumia kawi safi isiyochafua mazingira.

Gari lake amelipa jina Gadget Man Hybrid Car na upande wa mbele ameandika kwamba ndilo gari la kwanza linalotumia mitambo ya sola Kenya.

Anasema amekuwa na ndoto kuu ya kuwa mmiliki wa gari kwa muda mrefu lakini hakuwa na pesa.

"Sikuwa na pesa za kununua gari lakini niliketi chini na kukumbuka kwamba mimi ni mvumbuzi. Hapo ndipo nilipofikiria wazo la kuunda gari la kipekee, gari linalotumia mitambo ya sola na halihitaji mafuta," anasema.


Walter Mong'are: Je, ni kweli kuwa vijana Kenya wanabagua kazi?
Aligeuza ubaraza wake kuwa karakana kwa miezi minne na kuligeuza wazo lake hadi kuwa uhalisia.

Anakadiria kwamba ametumia takriban Sh125,000 (dola 1,250 za Marekani) kufanikisha mradi huo.

Bw Karumbo amesomea ufundi wa stima katika chuo hicho cha mafunzo anuwai cha Kitale.

Ameiomba serikali imsaidie kuunda magari zaidi yanayotumia nishati ya jua.

Wakenya mtandao wamekuwa wakimsifu kijana huyo na kuiomba serikali kuunga mkono juhudi zake.

Post a Comment

0 Comments