Waziri wa maswala ya kigeni wa Korea Kusini Kang Kyung
Image captionWaziri wa maswala ya kigeni wa Korea Kusini Kang Kyung

Korea Kusini imesema kuwa imeanza mazungumzo ya moja kwa moja na Korea Kaskazini wakati wa mkutano wa kieneo wikendi hii.
Waziri wa maswala ya kigeni Kang Kyung-wha alisema kuwa yuko tayari kuzungumza na mwenzake kutoka Pyongyang iwapo fursa itajitokeza.
Majaribio ya mara kwa mara ya makombora ya masafa marefu na yale ya kinyuklia yanayotekelezwa na Korea Kaskazini yameshutumiwa na majirani zake.
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupigia kura vikwazo vipya dhidi ya taifa hilo lililotengwa baadaye siku ya Jumamosi.
Mawaziri wa maswala ya kigeni kutoka muungano wa mataifa ya Kusini mashariki mwa Asia ASEAN wanakutana mjini Manila nchni Ufilipino.
Kitengo cha habari cha cha Korea Kusini Yonhap kimeripoti ''matarajio ya tahadhari'' kwamba Kang Kyung-wha atakutana ana Ri Yong-ho pembezoni mwa kikao hicho.
''Iwapo kuna fursa itakayojitokeza ni muimu kuzungumza'', bi Kang aliambia chombo hicho cha habari .
''Ningependa kuwasilisha tamaa ya kuitaka Korea Kaskazini kusitisha uchokozi na kuwasilisha ombi letu la mazungumzo yanayolenga kuweka utawala unaopendelea amani''.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson pia atahudhuria mazungumzo hayo ya wikendi ambapo mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini unatarajiwa kuwa ajenda kuu.
Wakati wa kuanza kwa mkutano huo wanachama wa mataifa ya ASEAN walitoa taarifa ya pamoja wakisema kuwa wana ''wasiwasi mkubwa kuhusu vitendo vya Korea Kaskazini , ambavyo vinahatarisha usalama''