Watanzania wahamasishwa kutumia Rajisi ya kwetu(Domain),kila mtanzania aanze kutumia .TZ mitandaoni
Akifungua mkutano wa Jumuiya ya watoa Huduma kwenye mitandao ulioshirikisha wamiliki wa Rajisi mbalimbali Africa kama .ke, .tz,.uk na nyingine Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani amesema kuwa Nchini ya Tanzania imekuwa nyuma sana katika kutumia Rajisi yake ya nyumbani ambayo ni .TZ ukilinganisha na mataifa yanayotuzunguka kama Kenya na mengine jambo ambalo linatajwa kuendelea kupoteza utambulisho wa Taifa letu katika mitandao.
Mkurugenzi Mtendaji wa TZNIC ambao ndio wanaohodhi Rajisi ya .TZ akizungumza na wanahabari kuhusu mambo mbalimbali yatakayojadiliwa katika mkutano huo |
Akizungumzia Rajisi ya Tanzania na matumizi yake amesema kuwa kwa sasa Rajisi ya .TZ ambayo ndiyo Rajisi maalum ya watanzania inatolewa na TZNIC ambao wanatoa kwa gharama za zisizozidi elfu 25 kwa mwaka ambapo amesema kuwa Gharama hizo ni kwa lengo la kusaidia kujiendesha wakati wanaanza kwa kuwa bado hawaajaanza kupata matangazo huku akiweka wazi kuwa kadiri muamko wa watanzania utakavyozidi kuwa mkubwa gaharama hizo zitapungua kwa kiasi.
Akizungumza nje ya Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa TZNIC ambao ndio wanaohodhi Rajisi ya .TZ Eng.Abibu Ntahigiwe amesema kuwa Lengo kuu la mkutano huo ni kujenga ushirikiano wa karibu baina ya wamiliki wa Rajisi afrika pamoja na kubadilishana uzoefu kuhusu maswala ya mitandao,ambapo mkutano huo unafanyika Tanzania ukiwa ni mkutano wa Tano kufanyika Barani Africa.
0 Comments