Breaking News:

Top Ad

//

Team Amplifaya imetolewa leo Waziri Makamba akishuhudia Ndondo Cup 2017


Alhamisi ya July 27, 2017 baada ya kuchezeshwa droo ya robo fainali ya michuano ya Ndondo Cup 2017, mchezo wa robo fainali ya kwanza kati ya Kibada One dhidi ya Vijana Rangers ulichezwa katika uwanja wa Kinesi.
Kibada One ni timu ambayo ilikuwa inaungwa mkono na kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM wakati vijana Rangers wao walikuwa wanasapotiwa na kipindi cha Amplifaya Meena Ally na Millard Ayo kwa bahati mbaya timu ya Millard na Meena ilifungwa katika mchezo wa robo fainali.
Vijana Rangers walifungwa na kwa mikwaju ya penati 4-2 hatua ambayo ilifikiwa kufuatia sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida wa dakika 90 huku licha ya Vijana Rangers kupoteza kwa penalti walionesha soka la kiwango cha juu.

Kutoka kulia mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Cup 2017 Shaffih Dauda akifuatilia mchezo na waziri wa mazingira January Makamba


Post a Comment

0 Comments