Breaking News:

Top Ad

//

Neymar amepigana na kususia mazoezi leo



Staa wa soka wa kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Neymar leo Ijumaa ya July 28 2017 ameingia kwenye headlines baada ya kugombana na mchezaji mwenzake Nelson Semedo wakiwa mazoezini.
Neymar katika video iliyonaswa mitandaoni imemuonesha akigombana na Nelson Semedo aliyejiunga na Barcelona kipindi hiki akitokea Benfica ya kwao Ureno, baada ya tukio hilo Neymar alisusia kufanya mazoezi na kuondoka zake.

Neymar na Semedo walipishana wakati wa mazoezi lakini Javier Mascherano aliingilia mvutano na Semedo aliendelea na mazoezi huku Neymar akiondoka, kwa sasa Neymar anahusishwa kuwa mbioni kuondoka FC Barcelona na kujiunga na PSG ya Ufaransa.

Post a Comment

0 Comments