Breaking News:

Top Ad

//

Alex Sandro kuvunja rekodi ya usajili Chelsea


SPORTS

Chelsea wanataka kumnnua beki wa Juventus Alex Sandro kwa kiasi cha fedha kitakacho vunja rekodi ya beki ghali zaidi kuwahi kusajiliwa katika ligi ya Uingereza.
Manchester  City  wamemsajili Kyle Walker pauni milioni 54 kutoka Tottenham lakini  Chelsea wanataka kuvunja rekodi hiyo kwa kutoa fedha nyingi kuliko iliyotelewa kwa Walker ili kumsajili Sandro kutoka Juventus.
Inasemekana Chelsea wameandaa kiasi cha £61m kwa ajili ya Sandro ambaye amekuwa akihitajika katika klabu hiyo kwa muda tangu Antonio Conte ajiunge na Chelsea.
Usajili wa Sandro kwenda Chelsea unaonekana kuwa mgumu kutokana na Juventusi kuwapoteza walinzi wawili Bonucci na Dani Alves  ambao wameondoka katika klabu hiyo hivyo inakuwa ngumu kwao kuruhusu kumpoteza mlinzi mwingine
Wakati huo huo kocha huyo wa Chelsea Antonio Conte ameamua kuongeza idadi ya wachezaji wa Kiingereza katika timu yake kutokana na uhaba wa wachezaji hao katika timu yake.
Conte amepanga kumnunua Ross Barkley kutoka Everton na Oxlade Chamberlain kutoka Arsenal ili kuongeza idadi ya wachezaji wa Uingereza ndani ya klabu hiyo. Mpaka sasa Chelsea wamekwishawasajili Timoue Bakayoko, Alvaro Morata na Rudiger lakini bado Conte anaona kuna uhitaji wa wachezaji wengine katika kikosi chake hicho.

Post a Comment

0 Comments